Dodoma FM

NaCoNGO yashauriwa kuwa daraja la kusaidia vijana kuchangamkia fursa za kilimo na ufugaji

13 July 2021, 12:48 pm

Na;Mindi Joseph .

Waziri Mkuu Mstaafu wa Tanzania Mh Mizengo Pinda amelishauri Baraza la Taifa la Mashirika yasiyo ya Kiserikali NaCONCO kuwa daraja la kusaidia vijana kuchangamkia fursa za kilimo na ufugaji.

Mhe.Pinda amebainisha hayo nyumbani kwake kijijini Zuzu Mkoani Dodoma baada ya kutembelewa na wajumbe wa Baraza la Taifa la Mashirika yasiyo ya kiserikali amesema vijana wana nafasi kubwa katika mchango wa taifa hivyo wanatakiwa kuchangamikia fursa zinazowazunguka hususan sekta ya kilimo.

Naye Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Mashirika yasiyo ya kiserikali Lilian Badi amesema hatua ya ziara hiyo wamejifunza mengi kuhusu masuala ya kilimo huku akitoa ombi la kuwezeshwa kiwanja kwa ajili ya ujenzi wa ofisi ya NACONGO.

Baadhi ya wajumbe wa Baraza la Taifa la Mashirika yasiyo ya kiserikali NaCONGO wameahidi kwenda kueneza ujumbe kwa vijana juu ya fursa za kilimo.

Baraza la Taifa la Mashirika yasiyo ya Kiserikali NACONGO lina mchango mkubwa kwa maendeleo ya jamii katika kuelimisha jamii kuondokana na hali ya umasikini.