Dodoma FM

Familia yaomba msaada ili iweze kumpeleka binti yao kwenye matibabu

12 July 2021, 12:12 pm

Na; Mariam Matundu. 

Wakazi wa Mkoa wa Dodoma wameombwa kumsaidia Rhoda Nhambali binti mwenye ulemavu wa afya ya akili ili aweze kupata matibabu. 

Bathromeo Nhambali ambae ni baba mzazi wa binti huyo amesema ulemavu huo ulisababisha kumkatisha masomo binti yake na sasa hali inazidi kuwa mbaya na amepata ulemavu mwingine. 

Amesema umasikini katika ngazi ya familia umepeleka kushindwa kumpeleka binti yake hospitali kwa ajili ya kupata matibabu na hivyo anaomba wanajamii  wamsaidie. 

Agnesi Galaghenga na Magreth Matandu ni majirani wa binti huyo wamesema amekuwa akipitia wakati mgumu na kusisitiza kuwa anahitaji msaada wa matibabu . 

Taswira ya habari imemtafuta Daktari wa magonjwa ya akili kutoka hospitali ya milembe jijini hapa Dkt.Samweli Motto ambapo amesema ni muhimu Rhoda akapelekwa hospitali ili kubaini tatizo hilo limetoka na nini.