Dodoma FM

Elimu itasaidia watoto kuripoti matukio ya ukatili wa kijinsia kwa urahisi zaidi

9 July 2021, 11:31 am

Na; Joan Msangi.

licha ya juhudi kubwa za serikali pamoja na mashirika mengne ya haki za binadamu kuendeleza upingaji wa vitendo vya ukatili wa kijinsia bado matukio hayo yanaendelea ambapo takribani watoto 40 elfu wanapitia hali hiyo.

Wakizungumza na taswira ya habari baadhi ya wananchi wamesema kuwa ni vyema sheria kali ikatolewa na pia watoto wapatiwe elimu ili iwe rahisi kwao kuripoti pindi tu wanapofanyiwa vitendo hivyo.

Nae Bi Jelda Luyangi kiongozi wa dawati la jinsia kwa watoto amesema kuwa endapo akibainika mtu kakiuka haki za watoto adhabu kali itolewe ili iwe mfano kwa watu wengine na pia ameeleza kuwa elimu izidi kutolewa kwa wananchi juu ya haki za watoto.

Ni vyema kuwalinda na kuwatunza watoto kwa sababu watoto ni Taifa la kesho.