Dodoma FM

Wakuu wa idara na taasisi watakiwa kuhakikisha wanalipa fidia kabla ya kutwaa Ardhi kwa wananchi

2 July 2021, 2:15 pm

Na;Yussuph Hans.

Marufuku imetolewa kwa wakuu wa idara, taasisi pamoja na wakurugenzi kuhakikisha wanalipa fidia kwa wananchi kabla ya kutwaa ardhi yao ikiwa ni pamoja na kuwepo kwa maridhio baina ya pande zote mbili.

Akizungumza katika kikao cha uzinduzi wa kampeni ya zero migogoro ya ardhi Mkoani Dodoma Waziri wa Ardhi Mh William Lukuvi, amesema kuwa kumekuwepo na utaratibu wa utwaaji wa ardhi za wananchi pasi na kupewa fidia au maridhiniano baina ya pande mbili suala ambalo huchochea migogoro kwa kiasi kikubwa.

Aidha ametoa tahadhari kwa wananchi kutokuwa na haraka ya kununua ardhi kwa madalali kutokana na kuwepo kwa matapeli wengi.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Jabiri Shekimweri amesema watawachukulia hatua kali za kisheria watu wote wanaofanya ujenzi kiholea.

Awali akifungua kikao hicho Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mh Antony Mtaka amesema kuwa migogoro watu wenye migogoro ambayo hajasuluhishwa na wamewahi kufikisha malalamiko yao katika ofisi mbalimbali wafike kwa ajili ya kusajili na kutatuliwa changamoto zao.

Kampeni ya zero migogoro inalengo la kuhakikisha mkoa wa dodoma unapunguza na kumaliza migogoro ya ardhi ambapo kampeni hiyo inadumu kwa muda wa siku 10, inayoanza jumatano July 5 ambapo katika siku 3 za mwanzo kampeni hiyo itafanyika katika ukumbi wa Jakaya Kikwete Convetion Center na siku zinazo baki kampeni hiyo itafanyika kwa kuwafata wananchi katika kata zao.