Dodoma FM

Wakazi wa Miganga walalamikia kukatika kwa maji mara kwa mara

2 July 2021, 11:53 am

Na; Benard Filbert.

Kukatika kwa maji kila mara katika mtaa wa miganga kata ya Mkonze mkoani Dodoma imetajwa kuwa kero kwa wakazi wa mtaa huo hali inayowalazimu kutumia maji ya visima ambayo sio salama kiafya.

Hayo yameelezwa na wakazi wa mtaa huo wakati wakizungumza na taswira ya habari ambapo wamebainisha kuwa kwa wiki maji yanaotoka mara moja kitendo ambacho hakikidhi mahitaji yao.

Wameongeza kuwa huduma ya maji kutoka mamlaka ya maji safi duwasa imekuwa ikipatikana mara moja kwa wiki hivyo kujikuta wakiacha kufanya shughuli za kiuchumi na kutafuta maji.

Rudovik Christian ni mwenyekiti wa mtaa wa miganga amesema ni kweli kuna changamoto hiyo lakini baadhi ya maeneo yameshindwa kupata huduma ya maji kutokana na kuwa kwenye muinuko.

Naye David Bochela diwani wa kata ya mkonze amesema licha ya baadhi ya maeneo kutokufikiwa na huduma ya maji bado kuna miradi itaendelea kutekelezwa ili kuondoa changamoto hiyo.

Kwa upande wake Sebastian Warioba amesema kupata maji kwa kipindi cha siku moja ndani ya wiki kunasababishwa na dharula katika matenki ya kuhifadhi maji.