Dodoma FM

Rasilimali za Taifa zikisimamiwa vyema zitanufaisha maisha ya kila Mtanzania

28 June 2021, 11:48 am

Na;Yussuph Hans.

Imeelezwa kuwa endapo Rasilimali za Taifa zitasimamiwa vizuri pamoja na kufanyia kazi mapendekezo ya mkaguzi na mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali zitanufaisha vyema Maisha ya kila Mtanzania.

Hayo yamebainishwa leo Jijini Dodoma na Mkurugenzi wa Taasisi ya WAJIBU Ludovick Otouh katika kikao cha uzinduzi wa ripoti ya uwajibikaji 2019/2020 ambacho kimewakutanisha wabunge, maafisa wa serikali pamoja na azaki.

Utouh amesema kuwa ripoti hiyo imefupisha masuala mbalimbali ambayo ni muhimu kwa taifa na kwa maslahi ya wananchi kuhusu rasilimali zao.

Aidha ametoa ushauri kwa serikali kuhakikisha wanasimamia vyema vyanzo mbalimbali vya mapato ili kudhibiti ufisadi ndani ya nchi.

Kwa upande wake mwakilishi wa ofisi ya azaki Charles Mpaka pamoja na Mbunge wa Mpwapwa George Malima wamepongeza taasisi ya wajibu kwa ubunifu wao wa uchambuzi wa ripoti za CAG, huku wakisema itakuwa chachu katika kuleta maendeleo ya taifa.

Uzinduzi wa ripoti ya uwajibikaji 2019/20 umefanyika leo Jijini Dodoma ukienda sambamba na mjadala wa Maoni kuhusu changamoto za mifumo ya TEHAMA katika kukuza uwajibikaji.