Dodoma FM

Jamii imetakiwa kufuatilia na kufahamu sheria ndogondogo za utunzaji wa mazingira

28 June 2021, 1:01 pm

Na; JOAN MSANGI.

Imeelezwa kuwa endapo jamii itafuatilia na kufahamu sheria ndogondogo za utunzaji wa mazingira itasaidia kwa kiasi kikubwa katika utunzaji wa mazingira pamoja na kuwa na mazingira bora.

Hayo yameelezwa na Bw.Dicksoni Kimaro Afisa Mazingira wa jiji la Dodoma wakati akizungumza na Dodoma Fm ambapo amesema sheria hizo zipo katika kila kata na tarafa hivyo ni wananchi wenywe wanatakiwa kuzifahamu ili kulinda mazingira.

Kwa upande wao baadhi ya wananchi wamesema kuwa serikai ingetilia mkazo suala hilo pamoja na kutoa elimu hii ingesaidia kwa kiasi kikubwa watu kuzifahamu sheria hizo jambo litakalo pelekea mazingira kuwa safi na bora kila wakati.

Suala la utunzaji mazingira ni jukumu la kila mwananchi na si la mtu mmoja mmoja hivyo serikali kupitia ngazi za chini kutoa elimu ya ziada kwa wananchi kuhusu umuhimu wake