Dodoma FM

Waathirika wa dawa za kulevya Nchini wasaidiwe

26 June 2021, 3:15 pm

Na;Mindi Joseph

Serikali imesema  tatizo la matumizi ya Dawa za kulevya Nchini limeendelea kuongezeka siku hadi siku huku akitoa Maelekezo mbalimbali  kwa kuwasiadia  waathirika wadawa za kulevya kiuchumi ili wasirudi katika matumizi ya Dawa hizo.

Akizungumza hii leo Jijini Dodoma na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi George Simbachawene kwaniaba ya Waziri Mkuu katika Maadhimisho ya Kilele Cha siku ya mapambano ya Dawa za kulevya ambayo Kitaifa yamefanyika Mkoani Dodoma ametaka kuangaliwa kwa mitaaala  ya Elimu kwa kuongeza somo la dawa za kulevya ili kuweza kuliokoa kundi la Vijana ambalo lipo hatarini katika matumizi ya Dawa za kulevya.

Awali akitoa taarifa kuhusiana na mapambano ya Dawa za kulevya ,Kamishina jenerali wa Mamlaka ya kuzuia na  kupambana na Dawa za kulevya Nchini,Gerald Kusaya ameeleza jitihada zinazofanywa na Mamlaka hiyo huku akieleza changamoto zinzazowakabili.

Naye Mkurungezi Mtendaji wa Shirika la Henry Jackson Foundation Medical Research International (HJFMRI) Sally Talike chalamila amesema wanashirikiana na mamlaka ya kudhibiti na kupambana na dawa za kulevya ili kuwasaidia waraibu wa dawa za kulevya pamoja na kudhamini kliniki 2.

Nao baadhi ya Waraibu wa Dawa za kulevya walikuwa na haya ya kusema.

Maadhimisho hayo yalianza rasmi Juni 23 ambapo Kilele chale kimehitimishwa Juni26 yakibebwa na kauli mbiu isemayo “Tuelimishane kuhusu tatizo la Dawa za kulevya kuokoa Maisha.