Dodoma FM

Asasi za kiraia zapongezwa mapambano dhidi ya dawa za kulevya

25 June 2021, 1:35 pm

Na; Benard Filbert.

Kamishna msaidizi wa kinga na huduma za jamii kutoka mamlaka ya kudhibiti na kupambana na dawa za kulevya Bi.Moza Makumburi amezipongeza asasi mbalimbali za kiraia zinazoshirikiana na Serikali kuzuia matumizi na biashara hiyo nchini.

Akizungumza na Dodoma fm amesema asasi za kirai zimekuwa na mchango mkubwa katika kupambana na matumizi ya dawa za kulevya ikiwepo utoaji wa elimu.

Amesema Serikali imejikita zaidi katika kutoa elimu kwa jamii juu ya athari za matumizi ya dawa za kulevya huku asasi hizi zikishiriki kikamilifu katika kuwaunga mkono katika utoaji elimu huo.

Aidha amesema kuelekea maadhimisho ya siku ya kimataifa ya kupambana na dawa za kulevya ambayo yanafanyika Viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dodoma wadau mbalimbali wanatoa elimu kwa wananchi namna ya kuepuka matumizi ya dawa za kulevya.

Amewataka wananchi kujitokeza katika viwanja hivyo ili kupata elimu namna ya kuepuka matumizi ya dawa za kulevya.

Maadhimisho ya siku ya kimataifa ya kupambana na dawa za kulevya duniani itaadhimishwa kesho Juni 26 jijini Dodoma huku mgeni rasmi akiwa waziri mkuu Mh.Kassim Majaliwa yakiambatana na kauli mbiu isemayo “Tuelimishane juu ya tatizo la dawa za kulevya,kuokoa maisha.