Dodoma FM

Wakuu wa wilaya wapya Dodoma wametakiwa kusimamia vema vipaumbele vya Mkoa

22 June 2021, 1:27 pm

Na;Yussuph Hans.

Mkuu wa Mkoa Dodoma Mh. Antony Mtaka amewataka wakuu wa wilaya aliowaapisha leo Jijini Dodoma kuhakikisha wanasimamia vyema Vipaumbele vya mkoa na kuleta mabadiliko Chanya.

Akizungumza baada ya hafla ya uapisho wa Viongozi hao, Mh Mtaka amesema kuwa Dodoma ina vipaumbele vyake kama Makao Makuu ya nchi na kuwataka Viongozi hao wakasimamie vyema vipaumbele hivyo.

Aidha amewaasa viongozi hao kuhakikisha wanatumia hekima na busara zao kuwatumikia wananchi na kuepuka migogoro isiyo na maslahi kwa taifa.

Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya kondoa Khamiss Mkananchi na Mkuu wa Wilaya ya kongwa Remedius Mwema pamoja wameahidi kufanya kazi kwa uadilifu huku wakiomba ushirikiano kutoka kwa wananchi.

Sanjari na mkuu wa mkoa wa dodoma Mh. Antony Mtaka amewataka viongozi wanaowatumikia wananchi kuhakikisha wanaheshimu msingi na heshima ya wana habari.

viongozi walioapishwa mapema leo jijini Dodoma ni mkuu wa wilaya ya kondoa Khamiss Mkananchi na Mkuu wa Wilaya ya kongwa Remedius Mwema ambao wanaungana na viongozi wengine walioteuliwa June 20, 2021.