Dodoma FM

Jamii imetakiwa kuimarisha Afya kwa kuzingatia inakula makundi matano ya chakula

22 June 2021, 11:55 am

Na; Benard Filbert.

Jamii imeshauriwa kuacha kusubiri ushauri katika suala la kutumia makundi matano ya vyakula na badala yake kujijengea tabia hiyo ili kuimarisha afya zao.

wito huo umetolewa na wakazi wa kijiji cha Solowu wilayani Chamwino mkoani Dodoma wakati akizunguma na taswira ya habari.

Wamesema kuwa suala la kula vyakula kwa kuzingatia makundi matano ya vyakula ni muhimu kwa kila mama mjamzito kwani humfanya kujifungua mtoto mwenye afya njema na kumuepusha na udumavu.

Aidha wameongeza kuwa jamii inapaswa kuacha kuishi kwa mazoea kwa kula vyakula vya aina moja kwani kufanya hivyo kunaweza kusababisha kukosa lishe bora.

Naye afisa lishe wa wilaya ya chamwino bi Bernadeta Petro amesema makundi matano ya chakula ni jambo ambalo linapaswa kuzingatiwa na kila mwananchi kwa faida yake binafsi na taifa kwa ujumla.

Aidha ametoa wito kwa jamii kuacha visingizio vya hali duni ya maisha bali watumie hata matunda ya asili kwa wale walio katika maeneo yanakopatikana.