Dodoma FM

Viongozi wametakiwa kuiga msimamo wa aliyekuwa Rais wakwanza wa Zambia

21 June 2021, 10:06 am

Na; Benard Filbert.

Viongozi katika nchi za Afrika wameaswa kuiga msimamo wa aliyekuwa rais wa kwanza wa Zambia Keneth Kaunda ili waweze kukuza uchumi katika mataifa yao.

Hayo yameelezwa na mhadhiri mchambuzi wa masuala ya kisiasa kutoka chuo kikuu cha Dodoma Bw.Paul Luisulie wakati akizungumza na taswira ya habari kuhusu mchango wa buriani Keneth Kaunda katika siasa za afrika.

Amesema mwendazake Keneth Kaunda atakumbukwa kwa mengi katika siasa za afrika ambapo viongozi wa mataifa mbalimbali wanatakiwa kumuenzi kwa kuiga msimamo wake ambao ulichangia kuipatia Zambia uhuru.

Kadhalika amesema kufutia kifo cha aliyekuwa rais wa kwanza wa Zambia Afrika imepoteza moja ya viongozi walioleta mapinduzi katika kutafuta uhuru.

Mwasisi wa Taifa la Zambia Kenneth Kaunda alifariki dunia June 17 akiwa anapatiwa matibabu ambapo amefariki akiwa na umri wa miaka 97.