Dodoma FM

TANAPA yaja na mkakati wa kuongeza watalii wa ndani kupitia vyombo vya habari

19 June 2021, 1:19 pm

Na;Mindi Joseph.

Shirika la Hifadhi ya Taifa TANAPA limejipanga kuongeza idadi ya watalii wa ndani na nje ya nchi Katika miaka mitano ijayo kupitia Vyombo vya Habari kuhamasisha wananchi kufanya utalii wa ndani.

Tanzania ni nchi ambayo imejaliwa kuwa na vivutio mbalimbali katika kuendelea kuhamasisha utalii wa Ndani Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Uhifadhi Dodoma Ahmed Mbugi amekutana na waandishi wa habari jijini Dodoma ili kuandaa mkakati wa kutangaza Utalii wa ndani .

Aidha, Mbugi amesema baadhi ya wananchi wanaamini kuwa kutembelea vivutio vya utalii ni lazima waende hifadhi za Taifa lakini katika Mkoa wa Dodoma na maeneo jirani vipo vivutio ambavyo wanaweza kwenda kuvitembelea.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Shirika la Hifadhi ya Taifa TANAPA Pascal Shelutete anasema moja ya utekelezaji wa majukumu ya shirika hilo ni kuihamasisha  jamii kutambua kuwa Utalii wa ndani ni muhimu.

Naye Jully lyimo Afisa Uhifadhi Mkuu wa Hifadhi za Taifa TANAPA amesema utalii husaidia kukuza uchumi na kipato kwa taifa pamoja na kuongeza ajira.

Shirika la TANAPA limejipanga kuongeza idadi ya watalii wa ndani na nje ya nchi Katika miaka mitano ijayo kupitia kutembelea hifadhi zake 22 zilizopo nchini.