Dodoma FM

Ole Sabaya afikishwa mahakamani

4 June 2021, 2:06 pm

Leo Juni 4, 2021 aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro, Lengai Ole Sabaya na wenzake wanne wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha kujibu tuhuma zinazowakabili.

Hayo yanajiri ikiwa ni siku chache zimepita baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kumsimamisha kazi ili kupisha uchunguzi wa tuhuma mbalimbali zinazomkabili.

Taarifa iliyotolewa Alhamisi ya Mei 13, 2021 na Mkurugenzi wa mawasiliano ya Rais Ikulu, Gerson Msigwa ilieleza kuwa, Sabaya alisimamishwa kazi kuanzia tarehe hiyo.

Sabaya anakabiliwa na tuhuma za Rushwa,Utakatishaji fedha,Unyang”anyi wa kutumia silaha na Kuongoza magenge ya uhalifu.
Kesi imeahairishwa hadi juni 18 .