Dodoma FM

Wakazi wa chitelela wakabiliwa na changamoto ya uhaba wa maji

2 June 2021, 9:27 am

Na; Victor Chigwada.

Wananchi wa mtaa wa chitelela Kata ya Nzuguni Jijini Dodoma wameendelea kukabiliwa na changamoto ya kukosa huduma ya maji safi na salama kwa muda mrefu.

Wakizungumza na taswira ya habari baadhi ya wananchi wa eneo hilo wamedai kutumia maji ya kisima ambacho kipo umbali mrefu hivyo wameiomba Serikali iwasaidie kuwachimbia kisima kimoja tu cha maji safi .

Nae mwenyekiti wa mtaa wa chitelela Bw.Samweli Robati amekiri wananchi wake kutumia maji ya kisima yanayo patikana umbali mrefu toka katika makazi ya watu hivyo ameiomba mamlaka ya maji safi na usafi wa mazindira DUWASA kuwasaidia kutatua kero hiyo.

Taswira ya habari ilizungumza na Diwani wa Kata ya Nzuguni Bw.Aloyce Luhega yeye amesema licha ya mwaka jana kata hiyo kuchimbiwa kisima kisima lakini bado maji hayo hayakidhi mahitaji ya wakazi wa eneo hilo.

Wizara ya maji imetenga zaidi ya bilioni 680.3 kwa mwaka wa fedha 2021/2022 ili kuhakikisha huduma ya maji nchini kutoka kwa asilimia 70.1 hadi 72.3 vijijini na asilimia 84 kwa mijini