Dodoma FM

Serikali yaweka mkakati wa kumaliza vikwazo vya biashara na Kenya

2 June 2021, 9:55 am

Na; Mariam Matundu.

Serikali kupitia wizara ya viwanda na biashara imeweka mikakati ya kuhakikisha inamaliza vikwazo vya kibiashara kati ya nchi ya Kenya na Tanzania ili kuimarisha biashara kati ya nchi hizo mbili.

Hivi karibuni kumekuwa na mikutano kati ya Kenya na Tanzania ili kumaliza vikwazo vya kibiashara ambavyo vimesababisha zaidi ya tani laki mbili za mahindi kutoka Tanzania kuharibika kwa kushindwa kuvuka kwenda Kenya kwa ajili ya masoko ,ambapo mpaka sasa vikwazo 34 kati ya 64 vimetatuliwa.

Mwandishi wetu Mariam Matundu amefanya mazungumzo na naibu waziri wa viwanda na biashara Exaud Kigahe na ameanza kwa kumuuliza, Serikali imeweka mkakati gani kuhakikisha vikwazo hivi havijirudii tena?