Dodoma FM

Serikali imeongeza bajeti ya fedha kwaaji ya wakala wa barabara za mjini na vijijini TARURA

1 June 2021, 2:10 pm

Na;Yussuph Hans.

Serikali imeongeza bajeti kwa Wakala wa Barabara za Mjini na Vijijini TARURA kwa mwaka wa fedha 2021/22 kwa ajili ya matengenezo ya Barabara maeneo mbalimbali Nchini.

Hayo yamebainishwa leo bungeni na Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mh Festo Dugange wakati akijibu swali la Mbunge wa Tabora Mjini Mh Emanuel Mwakasaka aliyehoji nini mkakati wa serikali kukarabati barabara zilizoharibika maeneo ya vijijini.

Mh Dugange amesema kuwa serikali imeongeza bajeti ya TARURA kwa mwaka huu wa Fedha ili kufanya matengenezo ya barabara za vijijini kwa awamu mbalimbali.

Mh Dugange amongeza kuwa hakuna sababu ya kuunganisha TARURA na TANROADS katika utendaji kazi na kwamba taasisi zote zinafanya kazi kwa kushirikiana.

Aidha amesema kuwa Serikali inaendelea kufanya tathmini katika kupandisha hadhi Barabara ambazo zinataji kusajiliwa na TANRODS.

Bunge limeendelea leo Jijini Dodoma ambapo Wizara mbalimbali zimewasilisha makadirio na mapato yake na hapo jana Wizara utamaduni sanaa na michezo iliwasilisha Bajeti yake kwa Mwaka wa Fedha 2021/22.