Dodoma FM

Viongozi wa Dini waombwa kuimarisha mafundisho ya kiroho

31 May 2021, 3:36 pm

Na;Yussuph Hans.

Wito umetolewa kwa Viongozi wa dini kuendelea kuimarisha Malezi na mafundisho ya kiroho ndani ya jamii ili kuepusha mmomonyoko wa maadili na kujenga kizazi bora.

Wito huo umetolewa na wakazi jijini hapa wakati wakizungumza na taswira ya habari kufuatia kuwepo kwa baadhi ya viongozi wa kidini ambao wamekuwa wakifanya vitendo vinavyokiuka maadali.

Wamesema kuwa licha ya kuwepo kwa viongozi ambao sio waadilifu kiimani, bado jamii inahitaji mchango wa viongozi wa kidini kwa ajili ya kurudisha taswira ya kuheshimika kwa dini pamoja na kuwa na jamii yenye maadili.

Kwa upande wao viongozi wa kidini wamekiri kuwepo kwa baadhi yao wanaotoa mafundisho yanayochafua haiba ya imani, na kuitaka jamii kuwa makini nao na kufuata mafundisho yaliyo mema.