Dodoma FM

Kata ya mpalanga yakabiliwa upungufu wa vyumba vya madarasa katika baadhi ya shule zake

28 May 2021, 1:34 pm

Na; Victor Chigwada.

Baadhi ya Shule katika Kata ya Mpalanga Wilayani Bahi zinakabiliwa na upungufu wa vyumba vya madarasa hali inayokwamisha maendeleo ya wanafunzi darasani.

Wakizungumza na taswira ya habari baadhi ya wananchi hao wamesema walianzisha ujenzi wa vyumba vya madarasa ambavyo kwa sasa havijapauliwa kutokana na kuishiwa fedha ambapo wameiomba Serikali kuwasaidia ili kukamilisha ujenzi huo.

Mwenyekiti wa Kijiji cha Mpalanga Bw.Mnyukwa Sakaila ameishukuru Halimashauri kwa kuwasidia ujenzi wa baadhi ya vyumba lakini amekiri kuwa ujenzi waliounzisha kwa nguvu za wananchi umeshindwa kukamilika.

Naye Diwani wa Kata ya Mpalanga Bw.Baraka Ndahani amesema tayari wameshafanya mchakato wa kuomba fungu la fedha kutoka Halmashauri ili kukamilisha ujenzi huo kwa shule za Vijiji vya Mpalanga na Chidilo.

Uboreshaji wa miundombinu ukiwemo vyumba vya madarasa umekuwa ni moja ya mahitaji makubwa kwa shule nyingi nchini kutokana na ongezeko la watoto wanaodahiliwa.