Dodoma FM

TARI watoa ushauri kilimo cha mihogo

26 May 2021, 1:15 pm

Na; James Justine

WATAALAMU kutoka Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI), wamewashauri wakulima wa zao la muhogo kufuata ushauri wa kitaalam kwa ajili ya kupata mazao bora na yenye tija.

Ushauri huo umetolewa na Mtafiti wa Mazao ya Mihogo na Viazi Vitamu, Festo Masisila, wakati akitoa ufafanuzi kwa wakulima kuzingatia mafunzo yanayotolewa na wataalam kwa mfumo wa shamba darasa kwa ajili ya kuwasaidia wakulima waweze kujifunza kwa vitendo.

Amesema kutokana na umuhimu wa muhogo wakulima nchini wanapaswa wajielekeze kulifanya zao hilo kuwa la biashara zaidi.