Dodoma FM

Auawa na ndugu tuhuma ya wizi

26 May 2021, 12:50 pm

Na; Thadey Tesha

Mtu mmoja ameuawa na ndugu zake wa karibu Wilayani Chamwino Mkoani Dodoma wakimtuhumu kujihusisha na vitendo vya wizi.

Akizungumza na waandishi wa habari hii leo kamanda wa Polisi Mkoani Dodoma SACP Gilles Muroto amemtaja marehemu kuwa ni Samson Lucas Kikoti 56.

Kamanda Muroto amesema pia wamefanya misako kwenye maeneo mbalimbali jijini Dodoma na kukamata watu wanaojihusisha na na vitendo mbalimbali vya kihalifu.

Aidha jeshi hilo linawashikilia watu wawili wakituhumiwa kuwapa mimba wanafunzi ambapo kamanda Muroto ametoa wito kwa jamii kuacha uhalifu kwani jeshi la Polisi halitawafumbia macho watakaobainika kujihusisha na vitendo hivyo.

Kwa upande wao baadhi ya wananchi jijini hapa wamelipongeza jeshi la Polisi kwa kazi kubwa wanayofanya ya kuhakikisha wanalinda usalama wa wananchi na mali zao kwa kukamata wahalifu.

Jeshi la Polisi limekuwa likifanya misako mbalimbali ambayo imefanikisha kukamatwa kwa watu wanaojihusisha na uhalifu ambapo limeitaka jamii kutoa ushirikiano katika mapambano hayo.