Dodoma FM

Wakazi wa kata ya makulu walalamikia kukosa huduma ya barabara

25 May 2021, 12:10 pm

Na; Ramla Shabani

Wananchi wa Mtaa wa Njedengwa Magharibi Kata ya Makulu  jijini Dodoma wameiomba Serikali kuwajengea daraja pamoja na kuwakarabatia barabara za mtaa huo.

Wakizungumza na taswira ya habari wananchi hao wamesema kuwa korongo linalopita mtaani hapo limekuwa likisababisha changamoto  msimu wa mvua kutokana na maji kujaa na kuzuia watu kuvuka.

Kwa upande wake mwenyekiti wa mtaa huo Daimu Haji amesema bajeti ya kutengeneza miundombinu hiyo imeshatengwa lakini tatizo limebaki kwa mashine ya kufanyia kazi hiyo.