Dodoma FM

Bei ya nguo za mitumba yashuka

25 May 2021, 11:20 am

Na; Tosha Kivula

Bei ya nguo za mitumba imeendelea kuwa ya wastani ikilinganishwa na miezi kadhaa iliyopita..

Wakizungumza na Taswira ya habari baadhi ya wanunuzi wa nguo hizo kwa bei ya reja reja wamesema bei hiyo imezidi kuwanufaisha ambapo kwa sasa wanaimudu pamoja na vipato vyao vya chini.

Nao wafanyabiashara  wa nguo hizo wamesema kutopanda bei kwa nguo za mitumba kumechangiwa na upatikanaji wake kutokana na mlipuko wa ugonjwa wa Covid-19 kupungua katika mataifa mbalimbali.

Nguo za mitumba zimekuwa zikitumiwa sana na wananchi wengi hususan wa kipato cha chini kutokana na kumudu gharama zake.