Dodoma FM

Chitela walalamikia kukosa elimu na vifaa vya uchimbaji wa madini ya chumvi

24 May 2021, 1:29 pm

Na; Victor Chigwada

Ukosefu wa elimu na vifaa vya kuchimbia madini ya chumvi na chokaa ni sababu kubwa inayo rudisha nyuma shughuli za uchimbaji.

Hayo yamesemwa na baadhi ya wananchi wanaojihusisha na uchimbaji wamadini hayo waliopo mtaa wa Chitela kata ya Nzuguni jijini Dodoma, wamesema ukosefu wa vifaa vya kisasa pamoja na utaalamu wa uchimbaji ndio kikwazo kikubwa kwao.

Mwenyekiti wa Mtaa wa Chitelela Bw.Samweli Robati amekiri kuwepo kwa changamoto hiyo ambapo amesmema wachimbaji wengi hutumia vifaa vya kienyeji hali inayochangia kukosa soko la uhakika.

Naye Diwani wa Kata ya Nzuguni Bw. Aloyce Luhega amesema kutokana na maeneo mengi ya machimbo kumilikiwa na watu binafsi,  baadhi yao wameyauza huku watu walioyanunua wakizuia zoezi la uchimbaji.

Baadhi ya wananchi wanaoishi karibu na maeneo yanakochimbwa madini ya aina mbalimbali wamekuwa  wakijishughulisha na uchimbaji kwa nia ya kujikwamua kiuchumi huku wengi wao wakiwa hawana utaalamu wowote juu ya uchimbaji.