Dodoma FM

madereva waaswa kuzingatia maadili ya muziki ndani ya vyombo vya usafiri

21 May 2021, 12:29 pm

Na; Shani Nicolous

Wito umetolewa kwa madereva wa vyombo vya moto kuzingatia maadili ya miziki inayopigwa pamoja na video katika vyombo vyao vya usafiri ili kutokuharibu mila na desturi za kitanzania.

Wito huo umetolewa na Bw. Leo Ngowi ambaye Kaimu Katibu Mtendaji wa Baraza la Ushauri Watumiaji huduma za Usafiri Ardhini LATRA CCC  wakati akizungumza na Taswira ya habari,ambapo amesema vyombo vya usafiri vimekuwa vikitoa huduma kwa watu tofauti na wa rika zote hivyo ni vyema maudhui yanayooneshwa yawe na staha.

Amewataka abiria kuzingatia mwendo wa dereva wakiwa safarini pamoja na kufunga mikanda, na wanaosafiri kwa kutumia pikipiki wazingatie uvaaji wa kofia ngumu ili kuepusha athari zinazoweza kujitokeza pindi wakiwa barabarani.

Dodoma fm imezungumza na wananchi jijini hapa ambao wamesema  nyimbo zilizokosa maadili zikipigwa katika vyombo vya usafiri huathiri baadhi ya watu hususani watoto.

Maadili mazuri ni msingi wa kumjenga mtu kimaisha hivyo ni vema wazazi , walezi na jamii kuzingatia nyimbo zenye maadili kutowapotosha watoto.