Dodoma FM

Wazazi waaswa malezi bora ya watoto

19 May 2021, 8:13 am

Na; Tosha Kavula

Jamii imetakiwa kufanya kazi pamoja katika kuhakikisha watoto wanapata malezi ya wazazi wote wawili kutokana na kuongezeka kwa wimbi la watoto kubadilika tabia..

Ushauri huo umetolewa na baadhi ya wazazi jijini hapa wakati wakizungumza na Dodoma Fm ambapo wamesema endapo mtoto watapata malezi ya baba na mama itamsaidia kukua kiakili, kimaadili pamoja na kiafya.

Wamesema ni vyema wazazi kuishi pamoja na kushirikiana katika jukumu la malezi mara tu wanapopata mtoto au watoto ili kuwajengea misingi iliyobora katika hatua zote za ukuaji wao.

Hii imetokana na baadhi ya wazazi kufarakana na kuacha watoto wakiteseka kwa kukosa malezi ya wazazi wote wawili ambapo hali hii imekua ikiathiri ukuaji wao.