Dodoma FM

Philip Mpango:viongozi watumie nafasi zao kwa uadilifu na maslahi ya taifa.

19 May 2021, 1:39 pm

Na; Yussuph Hans

Wakuu wa Mikoa wametakiwa kusimamia uchumi wa Nchi kwa kushughulika na Viongozi wazembe, kuheshimu Miiko ya kazi pamoja na kutatua Changamoto za Wananchi.

Akizungumza mara baada hafla ya uapisho wa Wakuu wa Mikoa na Wakuu wa Taasisi mbalimbali nchini, iliyofanyika leo Ikulu Dar es salam na kuhuhudhuriwa na viongozi mbalimbali, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Daktari Philip Mpango amesema ni vyema viongozi hao kutumikia nafasi zao kwa uadilifu na maslahi ya taifa.

Mh Mpango amesema kuwa kumekuwa na changamoto mbalimbali kwa Wananchi hivyo ni vyema viongozi hao wakawa sehemu ya kutatua changamoto hizo pasi na kutumia vibaya matumizi ya madaraka ikiwa ni pamoja kutenda haki.

Kwa upande wake Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, amesisitiza suala la viongozi kutambua wajibu wao pamoja na kushirikiana na viongozi wa ngazi za chini katika kusimamia na kuratibu makusanyo ya maduhuli.

Naye Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Job Ndugai amesema kuwa kumekuwepo na suala la ukiukwaji maadili katika taasisi ya TAKUKURU hivyo ni vyema viongozi walioteuliwa kushughulikia suala hilo huku akipendekeza kuwepo na ushirikiano kwa Viongozi wa Mikoa.

Sanjari na hayo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Samia Suluhu Hassani amefanya mbadiliko ya Wakuu wa Mikoa wawili akiwemo Mh David Kafulila ambaye aliyetueliwa kuwa mkuu wa mkoa wa Arusha, kwa sasa atahudumu Mkoa wa Simiyu, huku Mh John Mongela ambaye aliyetuliwa kuwa mkuu wa mkoa wa Simiyu, atahudumu katika Mkoa wa Arusha.