Dodoma FM

Biashara ya ulezi yashamiri jijini Dodoma

18 May 2021, 7:58 am

Na; Ramla Shabani

Baadhi ya wafanyabiashara wa ulezi jijini Dodoma wameelezea namna biashara hiyo inavyoshamiri kutokana na watumiaji wengi wa zao hilo wamesema kuwa zao la ulezi linatumiwa kwa wingi.

Wakizungumza na taswira ya habari wamesema kuwa watu wengi wanatumia ulezi kama lishe kwa watoto wao hali inayopelekea zao hilo kutoka kwa wingi.

Baadhi ya watumiaji wa zao hilo wamesema kuwa ulezi unafaida nyingi katika mwili wa binadamu kwakuwa inaimarisha kiwango cha sukari.

Aidha wamesema kuwa wanatumia zao hilo katika uji kama lishe kwa watoto.

Ulezi ni moja ya zao ambalo limejipatia umaalufu mkubwa ambapo watu wengi wamekuwa wakitumia katika uji kama mojawapo ya lishe kwa watoto.