Dodoma FM

Wakazi Makulu waomba wazazi wanao katisha watoto masomo wachukuliwe hatua za kisheria

11 May 2021, 8:24 am

Na;Benjamin Jackson.

Kutokana na kuzuka kwa tabia ya wazazi kusitisha masomo ya Watoto wao ya elimu ya sekondari pindi wanapo hitimu elimu ya msingi ,baadhi ya wananchi wameiomba serikali kuchukua hatua kali kwa wazazi wenye tabia kama hiyo.

Wakizungumza na taswira ya Habari baadhi ya wananchi wamesema ya kwamba Watoto hao pindi tu wanapositishiwa masomo yao ya sekondari wanajiingiza katika makundi yasiyo faa kama vile Watoto wa mitaani uvutaji bangi wizi na kadharika .

Wananchi wameiomba serikali kuunda sheria ndogo itakayo wabana wazazi pale wanapo shindwa kuwapa haki ya elimu kama msingi wa Maisha yao .

Kwa upande wao wazazi wameomba wapewe elimu ya kutosha hususani  maeneo ya vijijini, pia wameomba  ustawi wa jamii kutembelea maeneo mbalimbali ili kutilia mkazo suala la elimu ya sekondari na umuhimu wake kwa Watoto.

Taswira ya habari imezungumza na Bw .Leonard Ndama mwenyekiti wa mtaa wa Makulu jijini dodoma amesema kama mzazi asipo toa ushirikiano wa kumuendeleza mtoto katika suala zima la elimu ashitakiwe kisheria na kupelekwa kwenye baraza la kata .