Dodoma FM

Serikali kuimarisha na kufungua mipaka ya masoko katika Nchi za kanda ya Afrika mashariki na Maziwa makuu

11 May 2021, 11:15 am

Na;Mindi  Joseph.

Serikali imeahidi kuendelea kuwa na uchumi imara kwa kuimarisha na kufungua mipaka ya masoko katika nchi za kanda ya Africa mashariki na maziwa makuu.

Akizungumza katika Mahojiano na Taswira ya habari Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Exaud Kigahe amesema  moja ya changamoto ambayo imekuwa ikiwakabili wakulima baada ya kuvuna mazao yao ni kuyahifadhi ndani kwa muda mrefu hali inayosababishwa na kudorora kwa masoko hivyo Serikali imejipanga kuondoa changamoto hiyo.

Mh.Kigahe ameongeza kuwa Tanzania inasoko kubwa la mazao nchi za nje kwa kuwa nchi za Burundi, Rwanda, DRC na Sudan Kusini  zinahitaji mazao ya chakula hivyo serikali inaenda kuridhia mkataba wa masoko huru ya Africa.

Nchi za africa tayari zimeridhia mkataba huo ambao utaanza mwezi wa saba mwaka huu na endapo Tanzania pia itaridhia mkataba huo itasaidia kupanua wigo wa soko la mazao na kuvutia wawekezaji.

Naye Mwenyekiti wa Chama cha Wanawake Wafanyabiashara Dodoma (TWCC) Grace Kapesi amebainisha kuwa kuimarishwa kwa masoko  kutawawezesha wanawake wafanyabiashara  kufanya zaidi biashara zao  nje ya nchi.

Aidha mikakati ya Wizara yaViwanda na Biashara ni kuandaa sera ya ubora ili kuhakikisha uzalishaji wa ndani unazingatia ubora wa viwango kupitia mpango wa tatu wa miaka mitano wa maendeleo ya Taifa ambao unaushindani.