Dodoma FM

Serikali yaahidi kuwalinda wabunifu na wavumbuzi ili kuendelea kutengeneza ajira nchini

10 May 2021, 12:23 pm

Na;Mindi Joseph

Serikali imesema itaendelea kuwalinda wabunifu na wavumbuzi mbalimbali kupitia sheria ya alama ya biashara na huduma ya mwaka 2000 ili kuendelea kutengeneza ajira nchini.

Akizungumza na Taswira ya habari Raphael Mtalima Afisa utumishi na  utawala mwandamizi kutoka Brela idara ya miliki ubunifu amesema kwa mujibu wa sheria hiyo ya alama namba 326 pamoja na kanuni zake za mwaka 2000 zitaendelea kulinda haki zote za wananchi wabunifu na wavumbuzi kwa  maslahi yao na Taifa kwa ujumla.

Ameongeza kuwa Brela ni wadau wakubwa wa Mashindano ya Kitaifa ya Sayansi, Teknolojia na Ubunifu MAKISATU ambayo yanafanyika jijini Dodoma kwa mwaka 2021 ikiwa wao ni  wanasimamizi wa  sheria za miliki ubunifu Tanzania, wanaendea kuhakikisha sheria inatekelezeka vyema ili wabunifu hao waweze kufaidika.

Vijana wabunifu na wavumbuzi wamesama sheria ya mwaka 2000 inatekelezeka ipasavyo licha ya changamoto mbalimbali zinazowakabili ikiwemo kipato cha kuendeleza ubunifu na  vitu wanavyovivumbua.

Maendeleo ya sayansi na teknolojia hutegemea zaidi uvumbuzi na Ubunifu ili kuendeleza kukuza  teknolojia nchini na Vijana wengi wako na ujuzi mbalimbali lakini tatizo mfumo wa elimu unawadidimiza  wabunifu wengi.