Dodoma FM

Wakazi wa lugala watanufaika na elimu ya watu wazima

7 May 2021, 11:39 am

Na; Alfred Bulahya.

Wakazi wa mtaa wa Lugala kata ya Mbalawala  watanufaika na elimu ya watu wazima  baada ya uongozi  wa eneo hilo pamoja na wananchi kukubaliana kuanzisha  darasa ili kuwasaidia wananchi ambao hawakubahatika kusoma.

Akizungumza na Taswira ya habari mwenyekiti wa mtaa huo bw. Zefania Mgutwa amesema kupitia vikao na wananchi hao wamekubaliana kuanzisha darasa hilo kwa lengo la kuongeza uelewa kwa wakazi hao.

Amesema hatua hiyo imeungwa mkono kwa asilimia kubwa na wananchi wa eneo hilo kwani hadi sasa tayari zaidi ya wananchi 80 wameandikishwa huku wananchi arobaini (40)  tayari wameanza  kuhudhuria masomo.

 Wamesema endapo muitikio wa watu kujifunza utakua mkubwa wanampango wa kumueleza Afisa Elimu wa msingi  ili aweze kuzindua darasa hilo  hali itakayo ongeza hamasa kwa wananchi kujiunga na masomo hayo.

Nao wakazi wa mtaa  huo wameushukuru uongozi wa eneo hilo na wamesema wapo tayari kujiunga na kuwahamasisha wananchi wengine wasione aibu  wajiunge ili waweze kujua kusoma na kuandika.

Mtaa wa Lugala ni mtaa ulioko katika kata ya Mbalawala jijini Dodoma ni mtaa unao jitahidi kutatua changamoto za wananchi wake .