Dodoma FM

wananchi wahimizwa kutunza miundombinu ya maji na barabara

5 May 2021, 11:09 am

Na; Thadei Tesha

Wananchi jijini Dodoma wametakiwa kuendelea kutunza miundombinu ya maji na barabara ili iweze kutumika kwa muda mrefu kama ilivyokusudiwa.

Wito huo umetolewa na wenyeviti wa mitaa ya Kiwanja cha Ndege Bw.Ignas Rufyadira na Bi.Zena Chiuja ambaye ni mwenyekiti wa Mtaa wa Makongoro inapokarabatiwa barabara kwa  kiwango cha lami.

Wamesema miundombinu ya maji na barabara  imekuwa ikifanyika mara kwa mara ambapo wametoa rai kwa wananchi kuwa mstari wa mbele kuilinda na kuitunza ili iweze kuwanufaisha kwa muda mrefu.

Aidha viongozi hao wameiomba serikali kurekebisha mitaro ya maji taka ambayo imezidi kuwa kero katika mitaa hiyo ili kuepuka magonjwa mbalimbali kwani maji hayo yamekuwa yakitiririka hovyo mitaani.

Nao baadhi ya wananchi wa mtaa wa Kiwanja cha ndege na makongoro wameishukuru Serikali kwa kuwaboreshea miundombinu ya barabara hiyo baada ya kuwa mibovu kwa muda mrefu.

Mitaa ya Kiwanja cha Ndege na Makongoro ni miongoni mwa Mitaa ambayo serikali inaendelea kuboresha baadhi ya barabara za ndani kwa kiwango cha lami hivyo wananchi wametakiwa kuitunza na kuilinda.