Dodoma FM

Wafanyabiashara, wajasiriamali wapigwa msasa matumizi ya vipimo

4 May 2021, 1:40 pm

Na; Alfred Bulahya

Watumiaji wa vipimo mbalimbali jijini Dodoma wametakiwa kuhakikisha wanazingatia vipimo kwa mujibu wa sheria ili kuongeza thamani ya bidhaa zao.

Hayo yamesemwa leo jijini Dodoma na katibu tawala wa Mkoa wa Dodoma Bi.Aziza Muba, wakati akizungumza na wajasiriamali na wafanyabiashara mbalimbali katika semina na wadau hao wenye lengo la kutoa mafunzo ya utumiaji sahihi wa vipimo.

Akizungumza kwa niaba ya mkuu wa Mkoa wa Dodoma mgeni rasmi ambaye ni katibu tawala wa Mkoa wa Dodoma amesema kwa sasa Dodoma ina zaidi ya viwanda 3000 hivyo suala la uzingativu wa vipimo linapaswa kuanzia shambani kwa mkulima hadi kwa mlaji ili kuleta tija zaidi.

Aidha amesema kwa sasa Serikali imeanza kuandaa mpango wa kuanza kuuza mifugo kwa kupima uzito na sio kuangalia ukubwa wa umbo, ili kuongeza tija kwa wazalishaji na watumiaji.

Kaimu afisa mtendaji mkuu wa wakala wa vipimo Tanzania Bi.Stella Kahwa amesema ili kuelekea kwenye Tanzania ya viwanda wameamua kuandaa mafunzo hayo yatakayokwenda nchi nzima ili kuwafikia wafungashaji wadogo kufikia wa kati na hatimaye wa kimataifa.

Naye kaimu meneja wa wakala wa vipimo Mkoa wa Dodoma Bw.Karimu Zuberi amesema hali ya Mkoa huo imeendelea kuimarika katika suala la vipimo hivyo ni wajibu wa wadau na watumiaji wa vipimo kuzingatia maelekezo na miongozi inayotolewa ili kuepusha kuchukuliwa hatua ikiwemo kutozwa faini.

Baadhi ya wajasiriamali waliofika kupata mafunzo hayo wamepongeza hatua iliyofanywa na wakala wa vipimo huku wakiwashauri wenzao kuanza kuchukua hatua ya kubadilika na kuachana na tabia ya kuchezea mizani kwa lengo la