Dodoma FM

Wananchi Mbalawala waombwa kuchangia uboreshwaji maabara

3 May 2021, 9:59 am

Na ;Afred Bulahya.

Wakazi wa  mtaa wa Kawawa kata ya Mbalawala jijini Dodoma wameombwa kuchangia kiasi kidogo cha pesa kitakacho wezesha zoezi la uboreshaji wa maabara ya zahanati ya Lugala.

Wito huo umetolewa na mwenyekiti wa kamati ya afya ya mtaa huo bw. Stephano  Ngosi wakati akizungumza na taswira ya habari baada ya mkutano na wananchi wa mtaa wa kawawa uliofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita mtaani hapo.

Amesema maabara hiyo imekuwa ikikabiliwa na changamoto kutokana  na ubovu wa baadhi ya miundo mbinu hivyo kufanya wakazi wa eneo hilo kutumia gharama kubwa kwenda kutafuta huduma sehemu nyingine.

Katika mkutano huo wananchi na viongozi akiwemo mwenyekiti na mtendaji wa mtaa wamekubaliana kuchangia kiasi kisichopungua shilingi 1000 na kuendelea kwa kila mkazi ili kufanikisha ukarabati huo wa maabara.

Aidha wameiomba kamati ya afya kuhakikisha inafanya zoezi hilo kwa uwazi kwa kuhakikisha wanabandika majina ya watu wote watakaochangia ili kuepusha sintofahamu za kupotea kwa michango hiyo.