Dodoma FM

Zahanati ya Chanhumba yakabiliwa na ukosefu wa dawa

29 April 2021, 6:17 am

Na; Benard Filbert.

Wakazi wa Kijiji Cha Chanhumba Kata ya Handali Wilayani Chamwino wamelalamikia ukosefu wa dawa katika Zahanati ya Kijiji hicho hali inayowalazimu kununua dawa katika maduka ya dawa.

Hayo yameelezwa na wakazi wa Kijiji hicho wakati wakizungumza na taswira ya habari kuhusu changamoto ya upatikanaji wa huduma za afya inayowakabili.

Amos Chisima ni mkazi wa Kijiji hicho amesema mara nyingi wakienda kutibiwa katika Zahanati ya Handali hawapewi dawa huku wakielekezwa kwenda kununua kwenye maduka ya dawa.

Mwenyekiti wa Kijiji Cha Chanhumba Bw.Aidan David amekiri kuwepo kwa changamoto hiyo ambapo amesema tayari kamati ya dawa katika zahanati hiyo inaendelea kufanya upembuzi ili kuondoa usumbufu kwa wananchi.

Upatikanaji wa dawa umekuwa changamoto katika baadhi ya hospital pamoja na zahanati hali inayochangia usumbufu kwa wananchi.