Dodoma FM

Wananchi waomba kupatiwa elimu juu ya katiba

27 April 2021, 9:21 am

NA; Shani  Nicoalus               

Wananchi jijini Dodoma wametoa wito wa kupatiwa elimu juu ya katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 kutokana na kutoifahamu ipasavyo.

Hatua hii imefikiwa baada ya hivi karibuni Halmashauri kuu ya Chama cha mapinduzi CCM Mkoa wa Dodoma kuazimia kuwa katiba ya mwaka 1977 bado ina nguvu hivyo hakuna ulazima wa kufufua mchakato wa katiba mpya.

Wamesema kuwa wanatamani kuona wananchi wanapewa elimu juu ya katiba ya nchi hasa vijijini  ili kutambua faida haki zao, huku wakiongeza kuwa ni vema ikabaki kama ilivyo kwani ikibadirishwa kuna baadhi ya mipango haitatimia.

Halmashauri kuu ya Chama cha mapinduzi CCM mkoa wa Dodoma iliyokutana wiki iliyopita imeazimia kuwa katiba ya Jamuhuri ya muungano wa Tanzania ya  mwaka 1977 bado ina nguvu hivyo hakuna ulazima wa kufufua mchakato wa katiba mpya inayotokana na rasimu ya jaji  Warioba.

Akizungumza katika kikao hicho mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dodoma Godwin Mkanwa, amebainisha kuwa katiba hii inaweza kutupitisha salama. 

Hata hivyo Bw.Nkanwa amesema mwishoni mwa juma lijalo April 30 CCM Taifa itafanya mkutano mkuu maalumu jijini hapa ambapo Halmashauri hii ya mkoa inatoa neno kuelekea mkutano huo kwa wajumbe watakoshiriki.