Dodoma FM

Wakazi Handali walalamikia kukosa mtendaji

26 April 2021, 6:28 am

Na, Victor Chigwada.

Wananchi wa Kijiji cha Handali Wilaya ya Chamwino Mkoani Dodoma wametoa malalamiko yao ya kutokuwa na mtendaji hali inayochangia kurudisha nyuma maendeleo yao.

Baadhi ya wananchi hao wakizungumza na taswira ya habari wamesema kuwa kukosekana kwa mtendaji wa Kijiji kunasababishwa na mtendaji wao wa Kata.

Mwenyekiti wa Kitongoji cha  Kawawa Bw.Diksoni Muhaji amedai kuwa changamoto hiyo imesababishwa na mtendaji wa Kata na kuiomba Serikali iwapatie mtendaji wa Kijiji na kumbadilishia kituo cha kazi mtendaji wa Kata

Naye  Diwani wa Kata hiyo  Bw.Aidani Rubeleje amesema kutokana na ukosefu wa mtendaji huyo wa Kijiji wanalazimika kumtumia mtendaji wa Kata kukaimu nafasi hiyo katika Kijiji cha Handari kwa sasa.

Maafisa watendaji wa Vijiji ndio wasimamizi wakuu wa upangaji na utekelezaji wa mipango ya maendeleo katika Vijiji vyao huku wakisimamia utawala bora ndani ya jamii.