Dodoma FM

Kusudio la Rais Samia la kukutana na viongozi wa vyama vya siasa litasaidia kuimarisha maelewano.

23 April 2021, 10:24 am

Na; Benard Filbert.

Imeelezwa kuwa azma ya rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Samia Suluhu  ya kukutana na viongozi wa vyama vya siasa Nchini itasaidia kuleta maelewano baina ya serikali na vyama vingine vya siasa.

Akizungumza na Taswira ya habari  mchambuzi wa masuala ya kisiasa kutoka chuo kikuu cha Dodoma (UDOM) bw. Paul Luisilie Amesema kauli ya rais Samia ya kukutana na viongozi wa vyama vya siasa imetokana na mwenendo wa siasa ulivyo kwa sasa Nchini .

Aidha amesema endapo rais Samia atakutana na viongozi hao wa siasa  itasaidi kuimarisha vyama hivyo kwa kiasi kikubwa huku akiongeza kuwa ili chama cha siasa kiimarike kinahitaji majukwaa mbalimbali.

Jana rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Mh. Samia Suluh Hassan wakati akihutubia Taifa kupitia bunge alinukuliwa akisema katika kulinda uhuru wa kidemokrasia anakusudia kukutana na viongozi wa kisiasa nchini ili kuweka muelekeo wa pamoja wa kuendesha shughuli za kisiasa zenye tija.