Dodoma FM

Jamii yatakiwa kutambua kuwa haki sawa katika malezi itapunguza ukatili wa kijinsia

21 April 2021, 10:44 am

Na; Thadei Tesha.

Jamii imetakiwa kuhakikisha inatoa haki sawa katika malezi kwa watoto wao  wa   kike na wakiume ili kuleta usawa wa kijinsia na kupunguza vitendo vya ukatili kwenye jamii.

Wito huo umetolewa na afisa ustawi wa jamii Dodoma  Bi.Faudhia Shukuru Mohamed alipokuwa akizungumza na Dodoma Fm ambapo amewataka wazazi kuwalea watoto wao bila ubaguzi ili kujenga jamii yenye usawa.

Bi.Shukuru amesema  wamejitahidi kutoa elimu katika jamii ili kupunguza vitendo vya ukatili wa kijinsia  lakini bado kwa Mkoa wa Dodoma  vinaendelea katika baadhi ya maeneo.

Kwa upande wao baadhi ya wananchi jijini hapa wamesema elimu zaidi inahitajika katika jamii zao ili kupunguza vitendo hivyo.

Vitendo vya ukatili wa kijinsia vimekuwa vikishamiri katika baadhi ya jamii nchini ambapo vimesababisha madhara mbalimbali huku baadhi ya mila na desturi zikitajwa kuchangia kwa kiasi kikubwa.