Dodoma FM

Wananchi vijijini wanufaika na Elimu ya mfuko wa bima ya Afya CHF

20 April 2021, 11:49 am

Na; Benard Filbert.

Elimu iliyotolewa kwa wananchi wa maeneo ya Vijijini kuhusu mfuko wa bima ya afya CHF imesaidia kwa kiasi kikubwa  kuamsha hamasa ya  kujiunga na kutumia bima hiyo.

Hayo yameelezwa na mratibu wa bima ya afya CHF Mkoa wa Dodoma Dkt.Francis Lutalala wakati akizungumza na taswira ya habari kuhusu mwamko wa wananchi wa Vijijini kujiunga na mfuko huo.

Amesema kwa sasa mwamko umekuwa mkubwa ikilinganishwa na hapoawali ambapo watu wengi hawakutambua umuhimu wa kujiunga na mfuko wowote wa bima ya afya.

Aidha ameongeza kuwa wamekuwa wakitoa elimu kwa wananchi ambao wanajiunga na bima hiyo juu ya huduma ambazo wanaweza kuzipata kupitia CHF pamoja na hospital wanazoweza kutibiwa.

Ameongeza kuwa lengo la Serikali ni kuwapatia wananchi matibabu kwa gharama nafuu kupitia bima hiyo tofauti na bima zingine nchini.