Dodoma FM

Wafanyabishara Soko la Majengo, “bei za bidhaa hazijapanda”

20 April 2021, 12:42 pm

NA; RAMLA SHABAN

Wakati wafanyabiashara wa viazi vitamu jijini Dodoma wakisema bei ya zao hilo haijapanda katika mwezi huu mtukufu wa Ramadhan,wanunuzi wengi wameendelea kulalamikia kupanda kwa bei hizo.

Wakizungumza na Dodoma fm baadhi ya wafanyabiashara katika soko la Majengo  wamesema kuwa bado bei zimesalia zile zile na hazijapanda kama baadhi ya watu wanavyosema.

Nao baadhi ya wanunuzi  wamesema bei ya viazi vitamu haipo kama ilivyokuwa hapo awali na kwamba imepanda kwa kiasi fulani.

Viazi vitamu ni zao linalopatikana kwa wingi Mkoani Dodoma ambapo hata hivyo bei hupanda pale msimu wa uzalishaji unapofikia tamati.