Dodoma FM

Migogoro ya ardhi yapelekea Ndachi kukosa huduma nyingi za Msingi

20 April 2021, 11:27 am

Na; Mariam Matundu

Wakazi wa mtaa wa Ndachi jijini hapa wamekuwa na kilio cha muda mrefu juu ya migogoro ya ardhi pamoja na kukosekana kwa  miradi ya maendeleo katika mtaa huo.

Taswira ya habari imezungumza na baadhi ya wananchi wa mtaa huo ambapo wamesema mgogoro wa ardhi ni moja changamoto kubwa iliyodumu kwa muda mrefu ambayo imekosa Ufumbuzi.

Aidha mwenyekiti wa mtaa huo Bi Jocye Abel amesema mgogoro wa ardhi imekuwa ni chanzo cha matatizo mengine ndani ya mtaa wake hali ambayo imesababisha wananchi wa ndachi kupata mateso katika baadhi ya huduma za msingi.

Hata hivyo amesema tayari wamezungumza na mkuu wa wilaya pamoja na mkurugenzi wa jiji na wameahidi siku ya alhamisi tarehe 22 mwezi huu wanne watafika Ndachi na kushughulikia suala hilo.

Pamoja na hayo amewaomba Viongozi wa halmashauri ya jiji la Dodoma kumaliza  changamoto ya mgogoro wa aradhi ambao umedumu tangu 2016 mpaka leo  kutokana na hali hiyo kukwamishi maendeleo katika mtaa wake.

Mtaa wa ndachi ni miongoni mwa mitaa ya mkoani Dodoma ambo umeendelea kushuhudia mgogoro wa ardhi na kusababisha kukosekana kwa huduma muhimu ikiwemo Maji,Zahanati,barabara na Umeme.