Dodoma FM

(UDART) Mkurugenzi wa Fedha na Maendeleo ya Biashara asimamishwa kazi na Waziri mkuu

19 April 2021, 2:01 pm

Na;Mindi Joseph Chanzo

Waziri Mkuu Mh.Kassim Majaliwa amemsimamisha kazi Mkurugenzi wa Fedha na Maendeleo ya Biashara wa Wakala wa Mabasi yaendayo haraka nchini (UDART) Bi.Suzana Chaula.

Hayo yanajiri baada ya kufanya ziara ya kushtukiza katika kituo cha  karakana ya mabasi hayo na kukuta uharibifu wa mabasi 40 huku 100 yakifanya kazi kwa kusuasua.

Akizungumza akiwa katika karakana hiyo Waziri mkuu amesema, ndani ya miaka mitano aliyofanya kazi mkurungezi Mtendaji wa Mabasi hayo amechangia uharibifu na kusababisha hasara kubwa kwa Serikali.

Amesema kuharibika kwa mabasi hayo imechangia abiria wengi kukosa usafiri kwani wengi hawapandi mabasi hayo na kuendelea kudidimiza  mradi huo wa “UDART”.

Waziri Mkuu Majaliwa amesema ukosefu wa fedha ndani ya UDART umechangia kushindwa kununua  baadhi ya vifaaa vya kukarabati magari hayo 40 yaliyoharibika sababu ikiwa ni usimamizi mbaya.