Dodoma FM

Serikali yaombwa kupunguza bei nishati mbadala

19 April 2021, 11:43 am

Na; Thadei Tesha.

Mitambo ya gesi asilia

Gharama kubwa za nishati rafiki kwa mazingira ikiwemo gesi, zimetajwa kuchangia uharibifu wa mazingira kutokana na wananchi wengi kutozimudu.

Hali hii imechangia wananchi wengi kuendelea kutumia nishati ya mkaa na kuni ambazo zinasababisha uharibifu wa mazingira.

Wananchi jijini Dodoma  wamesema Serikali inapaswa kuhakikisha bei ya nishati ambazo ni rafiki kwa mazingira zinapatikana kirahisi ili wengi wao waweze kuzitumia.

sauti wakazi wa jiji la dodoma

Kwa upande wake afisa maliasili wa jiji la Dodoma Bw.Vedasto Mlinga amesema ofisi ya maliasili wameendelea kutoa elimu ya utunzaji wa mazingira kupitia viongozi wa Vijiji na Mitaa ambao nao wanaifikisha kwa jamii kupitia mikutano.

sauti ya afisa maliasili wa jiji la Dodoma

Ameongeza kwa kusema kuwa kila mwananchi anao wajibu wa kushirikiana na wadau wa mazingira pamoja na Serikali katika suala la utunzaji wa mazingira ikiwa ni pamoja na kufahamu athari zitokanazo na uharibifu huo.

sauti ya afisa maliasili wa jiji la Dodoma

Mara kadhaa Serikali imekuwa ikitoa elimu pamoja na kuhamasisha wananchi juu ya umuhimu wa utunzaji wa mazingira hivyo jamii imetakiwa kuzingatia  na kutumia fursa hiyo ipasavyo.