Dodoma FM

Waandishi tumieni kalamu zenu kuhamasisha maendeleo ya Nchi.

16 April 2021, 12:42 pm

Na; Benard Filbert.

Wito umetolewa kwa waandishi wa habari nchini kutumia kalamu zao ili kuhamasisha maendeleo ya Nchi na si vinginevyo.

Wito huo umetolewa na msemaji mkuu wa serikali na mkurugenzi wa idara ya habari maelezo Mh. Gerson Msigwa wakati akizungumza na wanahabari jijini Dodoma alipokuwa i akikabidhiwa ofisi na aliyekuwa msemaji mkuu wa serikali Dkt.Hassan Abbas.

Amesema katika kipindi chake hiki cha  kuiongoza Tasnia ya habari angependa kuona wanahabari wanakuwa vinara wa kuchochea maendeleo ya Nchi.

Mh . Msigwa amewahakikishia wanahabari kutoa ushirikiano wakati wowote watakapohitaji taarifa  kutoka serikalini.

Akikabidhi ofisi hiyo aliyekuwa msemaji mkuu wa serikal Dkt.Hassan Abbas amempongeza ndugu Msigwa kwa kuteuliwa kushika nafasi hiyo ambapo ameahidi  kumpa ushirikiano wakati wowote atapo hitaji.

Gerson Msigwa alikuwa mkurugenzi wa mawasiliano ikulu na hatimaye ameteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo na Msemaji Mkuu wa Serikali.