Dodoma FM

Serikali kuhamasisha wawekezaji ujenzi wa viwanda vya mbolea nchini

16 April 2021, 10:49 am

Na;Mindi Joseph .

Mkurugenzi wa mamlaka ya udhibiti wa mbolea Tanzania (TFRA) Dtk.Stephane Ngailo  amesema kuwa wataendelea kuhimiza na kuhamasisha wawekezaji kushirikiana na serikali ikiwemo kituo cha uwekezaji , kuwekeza katika ujenzi wa viwanda vya mbolea  hapa nchini .

Dkt.Ngailo ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na Taswira ya Habari ambapo amesema  mipango ya taasisi hiyo katika kipindi cha miaka mitano ijayo ni kuendelea kuwekeza katika viwanda vya mbolea pamoja na kutoa elimu kwa wakulima.

Ameongeza kuwa Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania inawafikia wakulima wadogo kwa kuhakikisha wanapata mbolea iliyo bora na kwa wakati.

Dkt Ngailo amesema kuwa wanaendelea kushirikiana na Serikali na kwa sasa wapo katika mchakato wa maandalizi ya kuapata mahitaji ya mbolea msimu 2021/2022

Mamalaka ya udhibiti wa mbolea Tanzania (TFRA) imeanzishwa kwa sheria ya  Mblolea No.9 ya mwaka 2009  huku ikitekelezwa kwa kanuni zilizotungwa mwaka 2011 na kuanza kufanya kazi mwezi Agosti,2012 ikiwa chini ya Wizara ya Kilimo.