Dodoma FM

ATCL yashauriwa kuajiri watu wenye ufanisi

9 April 2021, 1:02 pm

Na; Pius Jayunga.

Serikali kupitia shirika la ndege Tanzania ATCL imeshauriwa kuajili watu wenye taaluma ya maswala ya anga ili kuleta ufanisi katika utendaji kazi ulio bora ikiwa ni pamoja na kubadili mfumo wa manunuzi ndani ya Serikali.

Ushauri huo umetolewa na wachambuzi wa maswala ya kiuchumi, kisiasa na kijamii wakati wakiuzngumza na Dodoma Fm mapema leo kupitia kipindi cha Dodoma live ikiwa ni siku moja tu baada ya mkaguzi na mdhibiti  wa hesabu za serikali CAG kutoa ripoti ikionesha mwenendo wa matumzi ya fedha za umma.

Wachambuzi hao akiwemo Mhadhili kutoka chuo kikuu cha Dodoma (UDOM) Bw. Paul Luisilie amesema ni wakati sasa kwa Serikali kutoa fursa ya ajira kwa watu wenye utaalamu hasa katika sekta ya usafiri wa anga ili wakafanye kazi hiyo kitaalamu na kuepuka makosa yanayoweza kuzuilika 

Nae Mhadhiri kutoka chuo kikuu cha Iringa Profesa Enock Wiketye amesema ni muhimu kwa wabunge kuijadili ripoti ya CAG kwa umakini wakitambua umuhimu wa Taifa kuwa na usafiri wa ndege kwani ni chanzo moja wapo cha kukuza uchumi wa Taifa kwa kuzalisha ajira kwa wananchi na jukumu lililopo sasa ni kujifunza namna bora ya kuendesha mradi huo kwa faida.

Mapema hapo jana mkaguzi na mdhibiti mkuu wa hesabu za Serikali CAG Bw. Charles Kichele alitoa ripoti ya matumizi ya fedha za umma mbele ya vyombo vya habari alieleza kuwepo kwa ubadhilifu katika baadhi ya taasisi za Serikali ikiwemo shirika la ndege Tanzania ATCL ambalo kwa miaka mitatu mfululizo limekuwa likijiendesha kwa hasara.