Dodoma FM

Tanzania kujenga uchumi shindani wa viwanda

8 April 2021, 1:46 pm

Na; Mindi Joseph

Serikali imesema inaendelea na maandalizi ya mikakati ya utekelezaji wa mpango wa 3 wa maendeleo wa Taifa kwa kipindi cha miaka 5 unaolenga kujenga uchumi shindani wa viwanda kwa maendeleo ya watu.

Mapendekezo ya mpango huo yamesomwa  leo Bungeni Jijini Dodoma wakati wa kipindi cha maswali na majibu na  Waziri wa Fedha na Mipango Dk Mwigulu Nchemba ambapo amesema Mapendekezo ya mpango huo wa  Taifa wa miaka 5 kuanzia 2021/22 hadi mwaka  2025/26 umeandaliwa kwa kuzingatia dira ya taifa ya maendeleo na dhima ya kujenga uchumi shindani.

Dkt. Nchemba amesema tathiminina  ya  utekelezaji wa mpango wa 2 wa maendeleo ya Taifa wa miaka 5 uliopita unaonesha kuwa pato la taifa lilikua kwa asilimia 6.9 katika kipindi cha miaka mine(4).

Bunge linaendela kujadili na kuidhinisha mpango wa 3 wa maendeleo wa Taifa kwa kipindi cha miaka 5 kuanzia 2021 hadi mwaka  2025/26.