Dodoma FM

Hatimaye Soko la Sabasaba lapata uongozi

7 April 2021, 10:09 am

Na; Shani Nicolous

Katibu wa Soko la Sabasaba jijini Dodoma Bw.Isaka Nyamsuka amesema kuwa wamejipanga vyema kwa ajili ya kutatua changamoto mbalimbali  zinazowakabili wafanyabiashara.

Bw.Nyamsuka amesema kuwa tayari wameanza kuyatekeleza baadhi ya majukumu ikiwepo kusimamia usafi na kupanua baadhi ya njia ambazo zilikuwa hazipitiki.

Amewaomba wafanyabiashara kuwapa ushirikiano ili kufanikisha mipango yao kwa manufaa ya wafanyabiashara.

Kwa upande wao wafanyabiashara wa soko hilo wamesema wamekaa muda mrefu bila kuwa na viongozi hivyo wanatarajia changamoto zao kutatuliwa ndani ya muda mfupi.

Hivi karibuni wafanyabiashara katika soko la Sabasaba walipiga kura kuchagua viongozi wao baada ya kukaa kwa muda mrefu bila uongozi ambapo wana matarajio makubwa ya kuona mabadiliko chanya katika soko hilo.